Makosa yanayofanywa na wengi kwenye betting
Betting ni mchezo unahohitaji tahadhari kuwa na umakini pindi unapofanyika, kwasababu ni kitu kinachogusa uchumi na akili yako moja kwamoja, hivyo nimuhimu kufanywa kwa tahadhari kubwa na umakini wa hali ya juu. Hapa nimekuwekea makosa mablimbali yanayofanywa na watu wanaoshiriki michezo hii na jinsi ya kuepuka
Kutocheza kistaarabu
Watu wengi wamejikuta wakipoteza fedha nyingi sana kwa kushindwa kucheza kistaarabu, ustaarabu maana yake kucheza kiwango ambacho unaweza kukimudu endapo utapoteza, kucheza hovyo hovyo bila utaratibu kunaweza kukusabishia umskini na au kukuingiza katika madeni makubwa na msongo wa mawazo kila mara kumbuka kucheza kistaarabu.
Kutojua muda sahihi wa kupumzika au kuacha kabisa kubeti
Endapo betting inakuathiri sana kiuchumi kwakuwa unapoteza sana au inachangia kushuka kwa ufanyaji wako wa kazi nimuhimu kupumzika au kuaacha kabisa, ikiwa unashindwa kujidhibiti nimuhimu kutafuta msaada , hii itakusaidia kutoendelea kucheza na kuzidi kuathirika kiuchumi. Ikiwa unapoteza sana unatakiwa kupumzika na sio kukimbizana na hasara utaumia wewe
Kuifanya betting kama chanzo cha mapato
Kama ujuavyo betting ni mchezo na unapaswa kuwa sehemu ya starehe tu labda starehe isiyo starehesha kwa wakati mwingine, hivyo usiendekeze kubeti kuliko unavyoweza kufanya shughuli nyingine za kiuchumi. Hakikisha kiasi unachoweka kwaajili ya betting hakiathiri mahitaji mengine ya msingi, yani haipaswi kupewa kipaumbele kuliko unavyoweza kuzipa shughuli nyingine za kiuchumi kipaumbele. Hakikisha unabetia ziada na sio fedha za mahitaji ya msingi
Kujaribu kuokoa hasara uliyopata
Unapofanya betting au kucheza casino unaweza kupoteza sana kiwango kikubwa cha fedha , usifanye kosa la kujaribu kurudisha fedha uliyopoteza unaweza kujikuta unapoteza zaidi na kuumia , nimuhimu kukubali kukosea na kujirekebisha kuliko kujaribu kurudisha kiasi ulichokwisha kupoteza
Kutoa fedha kwaajili ya kulipa watu wengine wakupe michezo inayoweza kushinda
Mara zote unapaswa kufahamu kusninda ni bahati na hakuna anayeweza kujua matokeo kwa 100% jinsi yatakwavyokuwa , hivyo usitoe fedha kulipia tiketi kutoka kwa watu wengine. Unapaswa kujiuliza kama wana uhakika wa kushinda kwanini wao wasitumie mpaka wakuuzie wewe? ili kuepuka kupoteza fedha mara mbili unapaswa kujizuia kufanya kosa hilo
soma pia: Jinsi ya kujiunga meridianbet
Kutosoma sheria na masharti kabla ya kujisajili kwenye kampuni ya kubeti
Kusoma sheria na masharti ni jambo la muhimu sana japo wengi hupuuzia na kujikuta kupata madhara baadaye, kampuni za betting huwa na mashari na sheria mbalimbali mfano, kutoruhusu kuwa na account zaidi ya moja , KYC kuhitajika, kukuhitaji kutumia asilimia 100% ya dau uliloweka , sheria na masharti ya bonasi n.k, Ili kuepuka kosa hili nimuhimu kusoma sheria na masharti kabla ya kujiandikisha
Mwisho unahimizwa kucheza kistaarabu mara zote, na kucheza kiwango unchoweza kukimudu endapo unapoteza, jua muda sahihi wa kuacha au kupumzika. tukutane kwenye makala nyingine.