Fixed game kwenye betting ni matokeo yaliyopangwa au kunuliwa , matokeo hayo hayatarajiooowi kutokea tofauti baada ya mchezo kuisha. Tabia hii ya kununua michezo ipo lakini ni jambo haramu linalopigwa vita duniani kote. Jambo hili halikubaliki kwasababu sio tu lina shusha na kudidimiza mpira bali huathiri hata kampuni zinazotegemea matokeo ya mpira wa miguu. Ndiposa kampuni zote za michezo ya bahati nasibu zimejipanga kukabiliana na tabia ya kununua michezo au matokeo
Ukweli wa kwanza sio rahisi wewe kupata fixed game
Watu wengi wanadanganyika kuuziwa fixed game laikini ukweli nikwamba sio rahisi wewe fixed game kukufikia, unazokutana nazo ni predictions za kawaida ambazo zinaweza kushinda au kutoshinda, epuka kutapeliwa fedha ukidanganywa kuwa ni fixed game, wewe hauna uwezo wa kununua fixed game fixed game haiwezi kuuzwa kwa fedha ndogo kama milion 5 au 10 Kumbuka michezo hiyo inakuwa imeuzwa kwa fedha nyingi kwasababu ni hatari na inatakiwa kupatikana fedha ya kulipa timu nzima na aliyenunua hawezi kurisk kuonesha mchezo huo umenunuliwa. Epuka matapeli
Fixed game hazilipwi kwenye betting
Kampuni za betting huwekeza zaidi katika kudhibiti risk, na kama zingekuwa zinalipwa biashara ya betting isingewezekana. Wanayo mifumo ya ku detect na kutambua mchezo ulio nunuliwa kutokana na tabia za wateja miongoni mwa mambo mengine, hivyo kama utabahatika kukutana na fixed game mtandaoni hata kama utaijumuisha katika mkeka wako ufahamu fika kuwa mchezo huo hautalipwa, unaweza kuondolewa kabla baada au wakati ukiendelea epuka kupoteza fedha kwa kujindanganya ni fixed game
Kuna tofauti kati ya fixed game na predictions au sure tips
Watu wengi wanadhani predictions ndio fixed game, hivyo wanauziwa prediction ambazo kimsingi ni utabiri huku wakikwambia kuwa kuwa ni fixed game baadaye matokeo yanabadilika unakuwa umepoteza mara mbili. jiadhari sana kununua ticket mtandaoni tumia akili yako.
Mwisho kumbuka kucheza kistaarabu na kucheza kiwango unachoweza kukimudu.